04 November 2006

Huyu ni nani?

26 Comments:

At Sunday 5 November 2006 at 11:20:00 GMT, Blogger luihamu said...

Da'mija hapo nimechemsha.

 
At Monday 6 November 2006 at 11:26:00 GMT, Blogger Simon Kitururu said...

Huyu ni Cedella Marley Booker. Mama yake Bob Marley

 
At Monday 6 November 2006 at 21:36:00 GMT, Blogger Mija Shija Sayi said...

Nilikuwa naweka picha hii huku nikisema ngoja nimtege Mzee wa KILIMO (Ras Luihamu). Je ni kweli ulikuwa haumfahamu huyu?

Kitururu umepatia, Huyu ndiye mama Mzazi wa Mwanafalsafa Bob Marley.

 
At Tuesday 7 November 2006 at 04:51:00 GMT, Blogger luihamu said...

Namfahamu,lakini nilijua unanitega kwahiyo niliamuwa kukaa kimya.nimefurahi kama unamfahamu.Nilijua kama sio Simon,Ndesanjo watajibu.

 
At Tuesday 7 November 2006 at 04:53:00 GMT, Blogger luihamu said...

Naomba nikusahihisha sio mwanafalsafa bali ni NABII.

 
At Wednesday 8 November 2006 at 09:49:00 GMT, Blogger Rundugai said...

Ni Mama mzaa Chema,Hapo anasema dole Mwanangu kwa kunirusha,Ulale pema peponi Amina.
God Bless.
Jah People !

 
At Thursday 9 November 2006 at 14:56:00 GMT, Blogger Chesi said...

Dah! jamani naomba mnisamehe! mimi nilikuwa tayari naelekea kumuingiza kwenye ukoo wa mzee wetu marhum Chifu Adam Sapi Mkwawa...!

 
At Friday 10 November 2006 at 12:38:00 GMT, Anonymous Anonymous said...

Luihamu: nabii hawezi kuwa mwanafalsafa?

 
At Saturday 11 November 2006 at 07:38:00 GMT, Blogger luihamu said...

Mzee Ndesanjo,

NABII-ni mtabiri akiegemea katika dini.
MWANAFALSAFA- wanaegemea katika mambo ya kidunia.

Baada ya kuchambuwa nyimbo na misemo ya BOB,unakuta ya kwamba anaegemea katika neno la Mungu lilokuu katika yote,Bob anaegemea katika KILIMO kwasababu tukumbuke katika kitabu cha Mwanzo(BIBLIA)au katika vitabu vyote ndani ya Biblia hamna maelezo yoyote ya Teknolojia,hata wakati wanawamungu wanamtolea ZAKA,SADAKA walikuwa wanatumia MAZAO yaliyo toka shambani na kubarikwa na Mungu.Mzee Ndesanjo kama utapata muda soma kitabu cha Mwanzo.Wakati Mungu alimuumba ADAMU,alimweka katika BUSTANI,BUSTANI YA EDENI.Sasa basi Mzee Ndesanjo kwanini Mungu hakumtuma mwanadamu kuegemea na kuongozwa na mambo ya dunia kama teknolojia?

Naomba kukujibu yakwamba Nabii hawezi kuwa Mwanafalsafa.

N.B.Kama nitakuwa nimekosea usisite kunisahihisha.jah guidance.

 
At Saturday 11 November 2006 at 10:27:00 GMT, Blogger Mija Shija Sayi said...

Luihamu umesema katika biblia hakuna maelezo yoyote tekinolojia, je unafahamu kwamba mambo yaliyoandikwa katika biblia ni baadhi tu ya yaliyofanyika enzi hizo? Kuna mambo mengi sana hayakuandikwa na hii ni kutokana na uhaba wa tekinolojia wa kuhifadhi mambo uliokuwepo wakati huo.

Swali lingine, je Kilimo ni mambo ya dini au ya dunia?

 
At Sunday 12 November 2006 at 11:39:00 GMT, Blogger luihamu said...

Da mija

Kama Mungu aliweza kutenganisha mchana na giza,sembuse teknolojia?Kama Mungu aliweza kuumba dunia na mwanadamu sembuse teknolojia?Kwa mtazamo wangu Mungu aliona ni vizuri mwanadamu akavilinda na kuviheshi alivyo viumba.

Kilimo ni mambo ya dini kwa sababu,mwanadamu alikuwa anatoa zaka au shukrani kwa mwenyezi mungu kutumia mazao aliyovuna kama sadaka na kuomba Mungu azidi kumbariki.

Kama nimekose naomba unielimishe.

 
At Sunday 12 November 2006 at 12:26:00 GMT, Anonymous Anonymous said...

Luihamu:
Nadhani tatizo moja ni kuwa hatujafanya jambo moja muhimu sana. Hatujatafsiri maana ya neno teknolojia. Nimeona tatizo hili baada ya kuona ukisema kuwa kwenye biblia hakuna teknolojia. Kitabu cha Mwanzo ulichoniambia nilishakisoma mara nyingi. Na vingine vyote, na vile ambavyo vilinyofolewa kwenye biblia zamani. Kuna teknolojia kila mahali.

Mfano mdogo wa harakaharaka: Safina (chombo chenyewe na ujenzi wake) kwako sio teknolojia?

Iwapo tunafikiri kuwa teknolojia ni kompyuta tu basi ni kosa kubwa.

Da'Mija:
umesahau pale kwenye wiki kusema kama umeunga mkono Msangi Mdogo kuwa msimamizi au la.

 
At Sunday 12 November 2006 at 12:28:00 GMT, Anonymous Anonymous said...

Luihamu: blogu yako umeifuta au nini? Haipatikani.

 
At Sunday 12 November 2006 at 12:41:00 GMT, Blogger Mija Shija Sayi said...

Asante kwa kunikumbusha Ndesanjo.

 
At Sunday 12 November 2006 at 16:26:00 GMT, Blogger Simon Kitururu said...

Hivi biblia yenyewe inaweza kuwepo bila teknolojia?

 
At Sunday 12 November 2006 at 17:59:00 GMT, Anonymous Anonymous said...

Kitururu: swali zuri sana umeuliza maana naona tunataka kufanya kama vile maisha yanawezekana bila teknolojia. Jembe, ambalo Luihamu anapenda sana kulizungumzia, ni teknolojia. Kulikuwa na enzi yalitumika mawe, basi chuma kikagunduliwa, ikaja teknolojia ya jembe. Baadaye ikaja ya trekta.

Bila teknolojia ya uchapaji hiyo biblia anayozungumzia Luihamu sijui angeisomaje. Marasta wanalipinga sana kanisa katoliki, ni teknolojia ya kuchapa vitabu ya Guttenberg ambayo ilichangia kuangusha utawala wa kanisa hili. Teknolojia hii iliwezesha watu wa kawaida kuweza kuanza kusoma biblia na kuona jinsi gani wanadanganywa. Enzi zile maarifa yalionekana kuwa yanamilikiwa na viongozi wa dini.

Hata sasa teknolojia kama blogu, wiki, n.k. zinatusaidia watu wa kawaida kuweza kuwa na nguvu za kumiliki, kupeana, kusambaza maarifa tofauti na ilivyokuwa huko nyuma ambapo ilikupasa uwe fedha na mitaji mikubwa. Kamusi zilikuwa zikiandikwa na watu wanaitwa wasomi. Sasa mambo yanabadilika. Kama jinsi kisima cha maarifa kilihama toka kwenye himaya ya kanisa na kuhamia kwa wanazuoni na wenye vyombo vya habari enzi hizo, hivi sasa kunatokea mabadiliko mengine makubwa. Wigo unapanuka.

Najua Luihamu anapenda sana muziki wa rege, sasa bila teknolojia ya masuala ya kurekodi, santuri, na sasa CD, sijui ingebidi watu wafunge safari Jamaika kumsikiliza Bob akiimba chumbani kwake au?

Unajua wapo watu ambao wanatazama madhara ya teknolojia na kutishika sana. Teknolojia ndio zina madhara yake. Tazama teknolojia ya kanda za video jinsi ambavyo Osama anaitumia kutuma ujumbe kwa wafuasi wake na serikali anazozichukia duniani. Lakini teknolojia hiyo hiyo inaweza kutumia kutuma ujumbe kuhusu ugonjwa wa ukimwi.

Simu za mkononi zinatumika kufyatulia mabomu, lakini pia simu hizo zinatumika kupiga simu kwa dakitari au zimamoto ili waokoe maisha.

Najua kuwa teknolojia zina madhara yake. Madhara hayo hayajajengwa ndani ya teknolojia hizo bali yanatokana na tabia, hisia, na madhumuni ya watumiaji. Ila ufahamu huu haunizuii kuelekeza nguvu zangu kwenye kuendeleza mazuri ya teknolojia. Kwakuwa najua kuwa teknolojia zina mazuri, basi hapo ndipo ninaposimamia.

 
At Monday 13 November 2006 at 04:24:00 GMT, Blogger luihamu said...

Wakati namfundisha ndugu yangu jinsi ya kublogu na kumpa mfano hai blogu yangu na maelekezo alibonyeza DELETE BLOGU kwa bahati mbaya,mpaka sasa hivi najitahidi kufunguwa blogu nyingine.

 
At Tuesday 14 November 2006 at 04:31:00 GMT, Blogger Rundugai said...

Da'Mija Shija,gazeti tando la rastafarian limeungana na gazeti tando la kijiweni rundugai,kwa hivyo nitakuwa napatikana katika
www.rundugai.blogspot.com

karibu sana.

 
At Wednesday 15 November 2006 at 13:42:00 GMT, Blogger luihamu said...

Da'Mija,muungano wa Afrika unawezekana kama tukiungana sote na kushirikiana kwa pamoja.

 
At Wednesday 15 November 2006 at 15:56:00 GMT, Blogger luihamu said...

Da'mija soma shairi.bonyeza jina luihamu

 
At Wednesday 15 November 2006 at 22:29:00 GMT, Blogger MICHUZI BLOG said...

hata mie nilichemsha. nilidhania ni hayati tunu mrisho, msanii wa kuigiza aliyetutoka wiki iliopita. wamefanana kiasi...

 
At Friday 17 November 2006 at 02:24:00 GMT, Anonymous Anonymous said...

Da'Mija:
tatizo pale kwenye wiki tayari limetatuliwa!

 
At Sunday 14 January 2007 at 21:11:00 GMT, Blogger kingo said...

Naomba tuangalie maana ya neno teknolojia"Technology is the technical means people use to improve their surroundings. It is also a knowledge of using tools and machines to do tasks efficiently.


We use technology to control the world in which we live. Technology is people using knowledge, tools, and systems to make their lives easier and better.


People use technology to imrove their ability to do work. Through technology, people communicate better. Technology allows them to make more and better products. Our buildings are better through the use of technology. We travel in more comfort and speed as a result of technology. Yes, technology is everywhere and can make life better". pia nimeambatanisha ainisho la neno falsafa hapa "the study of seeking knowledge and wisdom in understanding the nature of the universe, man, ethics, art, love, purpose, etc.
www.carm.net/atheism/terms.htm" kwa mtazamo huo inaridhisha kuwa kwenye bibilia kuna falsafa na teknolojia pia, namuunga mkono bwana Ndesanjo,kun swali?

 
At Sunday 14 January 2007 at 21:14:00 GMT, Blogger kingo said...

Da Mija unsalimiwa na Stumai kutoka hapa ujerumani,Menard Mponda hajanijibu kama ninawezy kukutumia salamu zake,

 
At Saturday 20 January 2007 at 10:51:00 GMT, Anonymous Anonymous said...

mtu awaambie hawa watu mama ya bob alimzaa mtoto wa haramu na baba wa kizungu !
U gomvi mkubwa wa Peter Tosh na Bob ulikuwa Bob ame jump into band wagon ya uhuru wa watu weusi (ambao ulikuwa fashion wakati huo) watu wanayo haki ya kuuliza weusi wake !
Bob alikuwa na baba mzungu na sioni kwa nini yeye si mzungu !
However namshukuru kwakuwa alipigana sana vita yetu ingawa he was paid well for that any way.

 
At Wednesday 21 November 2007 at 14:04:00 GMT, Anonymous Anonymous said...

Oh bless.

 

Post a Comment

<< Home